Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameendelea
na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake siku ya leo Waziri
Makamba ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa
Rukwa.
Waziri Makamba
amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji
katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho
kimepungua hadi kufikia mita tatu. "Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa
kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na
kandokando ya ziwa, na ulishaji wa mifugo katika Vyanzo vya maji" Makamba
alibainisha
Katika ziara yake
baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia
kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za
matumizi ya maeno hayo zitaandaliwa ili kunusuru Ziwa Rukwa.
Pia,
wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa
zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalum
'beacons' ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwa zoezi hili lifanyike
haraka.
Aidha, Mhe. Makamba
amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa
Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa.
"nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa" Makamba
aliongezea.
Wakazi wa Mkoa wa
Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa
wanafunzi wa Primary na Sekondari kuwasili na miti na kutakiwa kuitunza mpaka
pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa
orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa
miti.
Katika hatua
nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali za dini na wazee wa
Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani, na kuahidi kugharimia Mkutano
wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo na kusisitiza agenda ya Mazingira iwepo.
Mkoani Rukwa Waziri
Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo
hayo na Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Nankanga ambapo wakazi wa maeneo
hayo wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974, Waziri
Makamba ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembele.
Chanzo: Ofisi ya
Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa pamoja na
Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wakielekea kutembelea fukwe za ziwa Rukwa
zilizoharibiwa vibaya.
Sehemu ya wakazi wa
Nankanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba (hayupo pichani) wakati wa Waziri akiwahimiza juu ya kutuza rasilimali
za Mazingira.
Mifugo ikichungwa pembezoni mwa Ziwa Rukwa Waziri
Makamba amegiza shughuli za aina hiyo kufanyika mita 200 kutoka kwenye chanzo
cha maji.
Sehemu ya Viongozi wa dini, siasa na wazee wa Mkoa wa Rukwa
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo
pichani) alipokutana nao na kusisitiza amani na Hifadhi ya Mazingira.




No comments:
Post a Comment